Rais Kenyatta leo amezuru kaunti za Mwingi na Embu
Published on: January 25, 2017 08:28 (EAT)
Audio By Vocalize
Rais uhuru kenyatta amepuuzilia mbali madai ya kinara wa upinzani Raila Odinga, kuwa serikali ina njama ya kuiba kura katika kinyang’anyiro cha mwezi agosti.
Kenyatta amemtaja Odinga kama mwanasiasa anayependa kulalamika na kuwachochea wafuasi wake, huku akidai ni ishara ya kuingiwa na kiwewe kabla ya uchaguzi mkuu.
Naibu wa Rais William Ruto akiwahimiza wafuasi wa jubilee kujisajili kwa wingi kama wapiga kura, na kuupiga kumbo mrengo wa upinzani ifikapo agosti. Francis Gachuri ana taarifa kamili.


Leave a Comment