Munya ahojiwa na PAC

Gavana wa Meru Peter Munya hatimaye alifika mbele ya kamati ya seneti kuhusu uhasibu kujibu maswali ya matumizi ya fedha katika kaunti hiyo. Munya aliwatetea magavana na kusema kuwa siyo lazima wao kufika mbele ya kamati hiyo na kuwa wanawezawakilishwa na mawaziri wa fedha katika kaunti hizo.

Munya alimshutumu seneta wa kiambu kimani wamatangi kwa kueneza uchochezi ya kukamatwa kw amunya alipozuru kaunti ya meru akiandamana na seneta wa Meru Kiraitu Murungi.

Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Kisumu Anyng’ Nyong’o, ailiipa kaunti ya meru siku mbili kuwasilisha stakabadhi sahihi, na kutakiwa kufika mbele ya kamati hiyo tena ijumaa wiki ijayo

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories