Alfred Keter Atusi Wafanyakazi Wa KENHA

Kulizuka kizaa zaa  katika kituo cha kupimia uzito wa malori ya kubeba mizigo eneo la Gilgil usiku wa kuamkia leo wakati ambapo mbunge wa Nandi hills Alfred Keter alipozua rabsha kudai kuachiliwa kwa lori la kuchimbia maji la mbunge maalum  wa chama cha URP Sonia Birdi. Keter ambaye alionekana kughadhabika sana aliwatusi maafisa waliokuwepo kazini katika kituo hicho. Video hiyo ambayo imesambaa sana katika mitandao ya kijamii kwa mara nyingine imetoa taswira ya namna viongozi wenye cheo cha kuitwa waheshimiwa wanaweza kutoa cheche za matusi kwa wale waliopwachagua na hata kukaribia kutumia mamlaka yao vibaya. Hii hapa ni picha zinazoelezea hali ilivyokuwa hapo jana usiku.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories