Christabel Ouko amezikwa nyumbani kwake Koru, Kisumu

Safari ya mwisho ya marehemu Christabel Ouko imefanyika hii leo nyumbani kwake huko Koru kaunti ya Kisumu. Marehemu ambaye ni mkewe aliyekuwa waziri wa mambo ya nje mwendazake Robert Ouko alifariki tarehe 21 mwezi huu kwenye ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Kisumu kuelekea Kericho baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o.
Jamaa na marafiki waliojawa na huzuni walifika nyumbani kwa Mwenda zake Mama Christabel Ouko ili kumpa heshima zake za mwisho.
Waombolezaji walimtaja Mama Ouko kama mtu aliyekuwa mcheshi mno na pia alikuwa mstari wa mbele kutetea elimu ya mtoto wa kike. Mazishi hayo yalihudhuiriwa na waziri wa mambo ya nje Amina Mohammed miongoni mwa viongozi wengine waliomuwakilisha rais Uhuru Kenyatta. Gavana mpya wa Kisumu Anyang Nyongo pia alikuweko.

Tags:

Christabel Ouko

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories