CORD yafuta maandamano ya tarehe 4 Januari

Muungano wa upinzani cord umefutilia mbali maandamano yao yaliopangiwa kufanyika kuanzia taerehe 4 januari mwaka ujao. Viongozi hao wakiwemo kinara wa wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula wamesema kuwa hatua hiyo imeafikiwa ili kuwaruhusu maseneta kupata maoni ya wananchi kuhusu vipengee tata katika sheria za uchaguzi.

Viongozi hao aidha wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwateuwa makamishana wa tume ya uchaguzi nchini iebc kwa haraka ili maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao yaanzishwe maepema.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories