EACC yamhoji Muraguri kuhusiana na ubadhirifu wa fedha

Katibu katika wizara ya afya Nicholus Muraguri adhuhuri ya leo alihojiwa na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi (EACC), kujibu maswali kuambatana na madai ya kupotea kwa mabilioni ya pesa katika wizara yake.
Duru za kuaminika ziliarifu Citizen nipashe kuwa mahojiano hayo yaliyochukua zaidi ya saa tatu yaliegemea ubadhirifu wa fedha na uhusiano wake na maafisa wengine katika wizara hiyo.
Na kama anavyoarifu Hassan Mugambi haya yanajiri huku mashirika ya kujamii yakipanga maandamano dhidi ya muraguri na waziri wa afya Cleopa Mailu.

Tags:

EACC cleopa mailu wizara ya afya Nicholas Muraguri

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories