Familia yalilia haki baada ya mtoto wao kunajisiwa

Familia moja katika kijiji cha Maiyuni huko Mwingi inalilia haki ya mtoto wao aliyenajisiwa tarehe 21 mwezi November. Inadaiwa kuwa aliyetekeleza kitendo hicho hajachukuliwa hatua licha ya kwamba familia hiyo ilipiga ripoti katika vituo vya polisi vya Mwingi na Nguutani. Na kinachoitia kiwewe familia hii ni ripoti kinzani kutoka hospitali ya mwingi level 4 na ile ya Nairobi womens. Moja ikionesha kuwa alinajisiwa huku nyingine ikionesha kuwa hakunajisiwa.

Tags:

rape mwingi nairobi womens

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories