Gavana na seneta wa Murang’a wakabiliana katika bunge la seneti

Gavana wa murang’a Mwangi Wa Iria na Seneta Kembi Gitura walishambuliana kwa maneno hadharani, walipokutana ana kwa ana katika kikao cha kamati ya uhasibu katika bunge la seneti. Kikao hicho kililazimika kuahirishwa ghafla, baada ya Wa Iria kukaidi kujibu maswali ya Gitura kuhusu ununuzi wa kipande cha ardhi, huku akidai seneta huyo alikuwa akipiga siasa na kumchafulia jina. Hata hivyo, Gitura, akiungwa mkono na maseneta wenzake alisisitiza Wa Iria hawezi kukwepa kupigwa darubini kuhusu matumizi ya fedha zilizogatuliwa.

Tags:

muranga kembi Gitura Mwangi Wairia

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories