IEBC yafutilia mbali cheti cha Wavinya Ndeti, kuwania ugavana
Published on: June 08, 2017 08:51 (EAT)
Chama cha Wiper kimepata pigo kubwa baada ya kamati ya IEBC kutupilia mbali cheti cha mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti. Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati imesema kuwa Wavinya Ndeti yuko katika vyama viwili vya Wiper na chama cha uzalendo kinyume na sheria. Uamuzi huo wa Chebukati unamaanisha kuwa chama cha Wiper hakitakuwa na mgombea ugavana Machakos kwani wakati wa kuwasilisha wagombea umefikia kikomo.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment