Kenyatta asisitiza msimu wa siasa umepita
Published on: December 12, 2017 09:04 (EAT)
Rais Uhuru Kenyatta leo ameliongoza taifa kusherehekea miaka 54 ya uhuru, huku akitoa wito wa amani na maridhiano baada ya mikwaruzano ya kisiasa ya takriban mwaka mzima. Hata hivyo Kenyatta ametoa tahadhari, haswa kwa vinara wa mrengo wa upinzani kuheshimu na kufuata katiba kikamilifu, huku akitangaza serikali haitasita kuuelekeza mjeledi kwa wale wanaoshinikiza za kujitenga kwa baadhi ya maeneo, kutokana na dhana ya kubaguliwa au kutengwa.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment