Kesi ya mahali pa kuhesabu kura za urais yasikizwa

Mahakama ya rufaa imeanza kusikiliza kesi iliyowasilishwa na tume ya uchaguzi nchini-IEBC, kupinga uamuzi wa mahakama kuu kuwa matokeo ya kura ya urais yatakayotangazwa katika maeneo bunge yatakuwa rasmi, na hayawezi kubadilishwa kwa njia yoyote na maafisa wa tume. Mawakili wa IEBC waliwaambia majaji watano wa mahakama ya rufaa kuwa uamuzi wa mahakama kuu ulikiuka taratibu za uchaguzi wa urais, kulingana na kipengee 138(3c) cha katiba. Hata hivyo, muungano wa upinzani-NASA unasisitiza upekuzi wa matokeo ya kura ya urais ni njama ya kuyakarabati.

Tags:

IEBC ballot papers James Muhati Lawy Aura

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories