Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yajadiliwa Seneti

Seneti imekubaliana na bunge la kitaifa kuwa uchaguzi ujao uhusishe matumizi ya vifaa vya elektroniki na njia mbadala iwapo vifaa hivyo vitafeli. Haya ni baada ya mjadala mkali uliofuatia kukosekana kwa wiano katika suala hilo baina ya wanakamati waliojukumiwa kutafuta maoni ya umma na kuwasilisha ripoti bungeni. Ripoti ya wengi imekubaliana na kauli ya bunge la taifa ila ikipendekeza kufafanuliwa kwa njia hiyo mbadala. Mrengo wa upinzani nao umewasilisha ripoti inayosisitiza njia ya kielektroniki pekee.

Tags:

sheria ya uchaguzi bunge la seneti

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories