Mahakama Kuu yafutilia mbali uchaguzi wa gavana wa Wajir
Published on: January 12, 2018 08:31 (EAT)
Uchaguzi wa gavana wa Wajir Mohamed Abdi umebatilishwa na mahakama hapa Nairobi, kufuatia kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake iliyowasilishwa na aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Ahmed Abdullahi. Jaji Alfred Mabeya amesema kuwa gavana wa sasa Mohamed Abdi hana cheti cha digrii hivyo haruhusiwi kushikilia wadhifa huo.