Mahakama ya rufaa ina wiki 2 kuamua ni nani anafaa kutangaza kura za urais

Majaji watano wa mahakama ya rufaa wana muda wa majuma mawili kuandaa uamuzi wao kuhusiana na kesi iliyowasilishwa na tume ya uchaguzi nchini-IEBC kupinga uamuzi wa mahakama kuu, kuwa matokeo ya kura ya urais yatakayotangazwa katika maeneo bunge 290 ni rasmi, na hayawezi kufanyiwa mabadiliko. Wakili wa IEBC, wenzao wa muunago wa upinzani-NASA na shirika la Katiba Institute wamehitimisha hoja zao mbele ya majaji wa mahakama ya rufaa, huku kila mmoja akishikilia msimamo wake.

Tags:

IEBC kura za urais mahakama ya rufaa

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories