Maji yapungua kwa kiwango kikubwa Ndaka-ini

Uhaba wa maji jijini Nairobi unazidi kuwahangaisha wenyeji kiasi cha kupigania maji kidogo yanayosambazwa na kampuni ya maji. Ni hali ambayo imewasababisha wenyeji kupunguza matumizi ya kila siku na kununua mitungi ya kuhifadhi maji. Mabwawa manne yanayotegemewa na wenyeji wa jiji yanaelekea kukauka, ikitizamiwa kuwa maji yaliyoko katika bwawa la Ndaka-ini, ambapo asilimia 84 ya maji hutoka, yatakithi haja za wakazi wa Nairobi hadi mwezi Aprili tu. Je, ni janga ambalo lingeweza kuepukika? Mwanahabari wetu Faiza Maganga anatupa taswira kamili.

Tags:

Ndakaini maji Uhaba wa maji Nairobi

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories