Makamishna wasema kuwa fidi ni ndogo
Makamishna wa tume ya uchaguzi nchini-IEBC wamekaidi pendekezo la serikali, kuhusu fedha wanazofaa kulipwa, kama fidia ya kuondoka ofisini kabla ya muhula wao kukamilika. Baadala yake, makamishna hao wametoa orodha ya marupurupu wanayoshinikiza kupewa. Na huku vuta nikuvute hiyo ikiendelea, kampuni ya royal media services imewasilisha kesi mahakamani, kuhimiza makamishna hao wasilipwe, hadi mzozo kuhusu gharama ya matangazo katika televisheni na radio, ambayo mwenyekiti wa IEBC Ahmed Issack Hassan na timu yake waliidhinisha utatuliwe.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment