Maseneta kujadili sheria tata za uchaguzi kesho
Published on: December 27, 2016 08:45 (EAT)
Maseneta wa mirengo ya Jubilee na Cord mchana kutwa wamekuwa kwenye mikutano ya kupanga mikakati, saa chache kabla ya kuandaliwa kwa kikao maalumu kujadili mapendekezo ya kupiga msasa vipengee kadhaa kwenye sheria za uchaguzi yaliyoibua utata. Na tofauti na kizaazaa kilichoibuka wiki jana katika bunge la kitaifa, maseneta wanasema watafanya kila juhudi kushawishiana kuhusu vipengee tata, bila ya kuvurugana wala kudhalilisha hadhi ya bunge.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment