Mchakato wa kumtafuta jaji mkuu mpya waendelea

Jaji wa mahakama ya rufaa Roselyn Naliaka Nambuye ametaja mswada uliodhinishwa jana na bunge kuzuia uhamiaji wa vyama vya kisiasa kama kinyume na katiba. Nambuye ambaye amehojiwa na tume ya huduma za mahakama ili kujaza nafasi ya jaji mkuu amesema kuwa katiba inawapa watu uhuru wa kujihusisha na vyama vyovyote wanavyotaka. Nambuye ni mmoja kati ya wanawake wawili ambao ndio pekee waliotuma maombi ya kutaka kumridhi Willy Mutunga.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories