Mtu mmoja afariki katika vurumai Bungoma
Published on: June 02, 2017 07:48 (EAT)
Mtu mmoja amefariki baada ya wafuasi wa gavana wa Bungoma Ken Lusaka kuvurugana na wale wa wapinzani wake wakuu Alfred Khangati wa ODM na Wyclife Wangamati wa Ford Kenya. Mwendazake alifariki kutokana na majeraha ya risasi, baada ya polisi kuingilia kati na kuyatawanya makundi ya wafuasi walioshambuliana, na kulemaza shughuli mjini Bungoma. Wale wanaozimezea mate nyadhifa za ugavana mchana kutwa wamewasilisha stakabadhi zao za uteuzi kwa tume ya uchaguzi nchini-IEBC.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment