Mwanahabari Agawo Patrobas aaga dunia

Mtangazaji mashuhuri wa Radio Ramogi inayomilikiwa na kampuni ya Royal Media Services, Agawo Patrobas ameaga dunia mapema leo katika hospitali ya Nairobi womens iliyoko jijini Nairobi.

Patrobas alizirai siku ya jumapili akiwa nyumbani kwake wakati akijitayarisha kufika kazini na baadaye akapelekwa hospitalini alikofariki akipokea matibabu.

Mwenye kiti wa shirika la royal media services, SK Macharia pamoja Naibu Mwenyekiti Mama Gathoni Macharia wameiongoza  jamii pana ya RMS kumuomboleza Agawo na kumtaja kuwa mtu aliyejitolea kikamilifu kutekeleza wajibu wake.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories