Mwenyekiti wa IEBC akutana na viongozi wa upinzani
Published on: February 08, 2017 08:17 (EAT)
Audio By Vocalize
Muungano wa upinzani umewashinikiza makamishna wapya wa tume ya uchaguzi nchini IEBC kuwafuta kazi wakurugenzi wawili wanaosimamia vitengo vya teknolojia (ICT) na usajili wa wapiga kura, kwa kile wanachodai ni ukosefu wa uwajibikaji. Katika kikao na makamishna wa IEBC, viongozi hao wa NASA pia wametaka hakikisho kuwa sajili ya wapiga kura itakayotumika katika uchaguzi wa mwezi Agosti itakuwa safi.


Leave a Comment