Naibu Rais aongoza mikutano ya Jubilee Nyamira, Kisii
Published on: July 13, 2017 09:08 (EAT)
Audio By Vocalize
Chama cha Jubilee kwa mara nyingine kimerejea kaunti za Kisii na Nyamira kusaka angalau kipande cha kura za eneo hilo, huku zikisalia siku 25 uchaguzi mkuu uandaliwe. Naibu wa rais William Ruto aliongoza pilka pilka za kuirai jamii ya Kisii kukumbatia kibwagizo cha Uhuru Tano Tena, huku akiorodhesha mafanikio ya Jubilee miaka minne, na kutoa msururu wa ahadi iwapo watafanikiwa kupata muhula mpya ikulu.


Leave a Comment