Raila aidhinishwa kugombea urais
Published on: May 05, 2017 09:10 (EAT)
Chama cha ODM kimeidhinisha uteuzi wa kinara wake Raila Odinga kupeperusha bendera ya muungano wa upinzani-NASA katika kinyang’anyiro cha mwezi Agosti. Katika kongamanao la chungwa lililohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 4,000 Odinga alitangaza kuwa safari yake ya kuwa Joshua imeng’oa nanga rasmi, huku akiorodhesha masuala ya kupunguza gharama ya maisha, kuwaunganisha wakenya na vita dhidi ya ufisadi kama mambo muhimu atakayoyapa kipaumbele iwapo atafanikiwa kuwa ndani ya ikulu mwezi Agosti.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment