Raila akutana na Chebukati

Utata unazidi kugubika maandalizi ya marudio ya uchaguzi wa urais, huku zikisalia siku sita kabla ya kinyang’anyiro hicho. Kinara wa NASA Raila Odinga leo amekutana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, na kukariri kuwa yuko tayari kurejea uwanjani, iwapo masharti aliyotoa yatatekelezwa. Licha ya serikali kuitangaza Alhamisi ijayo kama siku ya mapumziko, kuwawezesha wakenya kushiriki kwenye zoezi hilo, Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza mazungumzo yoyote kati yake na Odinga hayatagusia suala la kuahirisha uchaguzi huo.

Tags:

IEBC raila odinga Wafula Chebukati

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories