Ruto akemea upinzani kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wa IEBC

Naibu wa Rais William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kuacha kuingiza siasa katika shughuli ya uteuzi wa mwenyekiti na makamishna wa tume ya uchaguzi IEBC. Viongozi wa upinzani wanadai kuwa si sawa kwa Wafula Chebukati kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo kwani anatoka katika jamii moja na afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba. Ruto aliyasema hayo alipokutana na wajumbe kutoka kakamega waliomtembelea katika boma lake huko Sugoi kaunti ya Uasin Gishu.

Tags:

IEBC william ruto Wafula Chebukati

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories