Serikali ya Marekani yaonya dhidi ya ufisadi nchini Kenya

Serikali ya Marekani yaonya dhidi ya ufisadi nchini Kenya

Serikali ya Marekani imeonya dhidi ya ufisadi nchini huku ikizindua mpango wa shilingi bilioni 4.5 kuhusu usalama wa chakula katika kaunti ya Turkana.

Aidha soko la mifugo lililogharimu shilingi milioni 38 limefunguliwa mjini Lodwar na kutoa afueni kwa wafugaji.

Akizungumza wakazi wa uzinduzi huo, Balozi wa Marekani nchini Robert Godec amesema soko hilo litatoa nafasi ya kutoa mapato zaidi na kuimarisha hata biashara nyingine kwa wakaazi wa Lodwar.

Serikali ya Marekani pia inasaidia katika ujenzi wa masoko mengine 20 katika kaunti zilizo na jamii za wafugaji kaskazini mwa Kenya kwa lengo la kutoa usalama wa chakula.

Waziri wa ugatuzi na maeneo kame Eugene Wamalwa na Gavana wa Turkana Josephat Nanok walishuhudia uzinduzi huo.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories