UhuRuto kufanyia mabadiliko serikali yao
Published on: November 29, 2017 08:56 (EAT)
Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto sasa wamezamia mikakati ya kuunda baraza la mawaziri ambalo litamwezesha kutekeleza ruwaza yake na kadhalika kumfanikisha naibu rais kuweka mikakati ya kutafuta urais mwaka 2022. Wengi wa wale waliomuunga mkono Rais Kenyatta kuchaguliwa kwa muhula wa pili wakisubiri kwa hamu kujua hatma yao, mabadiliko katika baraza la mawaziri ni shughuli ambayo itawaacha baadhi ya mawaziri bila kazi huku wengine wakipata nafasi ya kuhudumu tena kutokana na utendakazi wao.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment