Utata wa kumteua mwaniaji urais wazuka
Published on: October 03, 2016 09:40 (EAT)
Je, muungano wa CORD uko sawa? Matamshi ya vinara wenza Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula yalitoa taswira ya mkwaruzano unaochochewa na kitendawili cha atakayepeperusha bendera ya mungano huo katika kinyang’anyiro cha urais mwaka ujao. Huku ikidaiwa Musyoka na Wetangula huenda wakang’atuka na kumwacha Odinga solemba, wadadisi wanadokeza kuwa itambidi Odinga kuipanga upya safu yake, ili kuimarisha nafasi yake ya kumbwaga Rais Uhuru Kenyatta mwakani. Je, mustakabali wa cord ni upi?
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment