Viongozi wa Jubilee wapinga shinikizo la kuivunja IEBC

Nipe nikupe imeibuka upya kati ya viongozi wa Jubilee na wenzao wa mrengo wa Nasa kuhusiana na usimamizi wa uchaguzi mpya wa urais katika muda wa siku 59 sasa. Huku kinara wa Nasa Raila Odinga akisisitiza mabadiliko makubwa katika tume ya IEBC, Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wanadai wapinzani wao wanatoa vijisababu tu, lengo lao likiwa ni serikali ya nusu mkate. Hata hivyo, Odinga amesisitiza hatarejea kwenye debe hadi maafisa wakuu sita wa IEBC wapigwe kalamu na kufunguliwa mashtaka.

Tags:

Uhuru kenyatta raila odinga JUBILEE IEBC Reforms

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories