Wajumbe wa Jubilee waanza kuwasili Nairobi

Msisimko unaendelea kukumba wanachama wa vyama tanzu vya Jubilee huku zikisalia saa chache kabla ya kung’oa nanga kwa kongamano la siku tatu litakalofikia kilele kwa kuvunjwa vyama hivyo na kuundwa kwa chama cha Jubilee Party.
Wajumbe wa vyama 13 vinavyonuia kuungana walianza kuwasili jijini Nairobi kutoka maeneo mbali mbali ya taifa hili, huku viongozi wa vyama hivi wakijitosa katika misururu ya mikutano kushughuklikia mapokezi yao.
Rais Uhuru Kenyatta tayari amekabidhiwa mfumo wa uchaguzi wa maafisa 77 wa vyama hivi, utakaozingatia uzito wa chama, maeneo na suala la jinsia miongoni mwa mengineyo.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories