Wazee wa Kirinyinyaga wajitenga na shughuli ya kumtawaza Waiguru
Published on: September 17, 2016 09:46 (EAT)
Kundi la wazee katika kaunti ya kirinyaga sasa limejitokeza na kujitenga na hafla iliyokuwa ya kumtawaza aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru hapo jana katika azma yake ya kuwania kiti cha ugavana cha Kirinyaga.
Wazee hao wanasema hafla hiyo ni kinyume na desturi za jamii yao, wakidai aliyemtawaza Waiguru alikuwa mtu binafsi na wala hakuwashirikisha kama ilivyodaiwa.
Aidha wanadai kuwa kulingana na mila na desturi zao lazima kiongozi apate Baraka za wazee ili wamfungulia njia kisiasa
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment