Rais Kenyatta akutana na watahiniwa wa KCPE

Rais Kenyatta akutana na watahiniwa wa KCPE

Rais Uhuru Kenyatta mapema leo alikuwa katika Shule ya msingi ya Uhuru gardens iliyoko mtaani Langata kuwatakia kila la heri watahiniwa wa KCPE. Uhuru amewahakikishia watahiniwa hao kwamba wote watajiunga na kidato cha Kwanza Mwaka ujao na kuwa mikakati yote ya kuhakikisha hilo linafaulu inawekwa. Rais alizuru madarasa kadhaa kuzungumza na wanafunzi katika siku ya pili ya mitihani hiyo. Waziri wa elimu Amina Mohammed, mwenyekiti WA baraza LA mitihani nchini KNEC Prof George Magoha, na Afisa mkuu WA TSC waliandamana na Rais.

latest stories