Rais Uhuru Kenyatta awafuta kazi mawaziri 13

Rais Uhuru Kenyatta leo amewatema mawaziri 13, na kuwasaza 6, kati ya wale waliohudumu katika baraza lake la kwanza la mawaziri. Katika tangazo lililowaduwaza wengi, rais hakuwajumuisha Amina Mohamed, Mwangi Kiunjuri, Eugene Wamalwa na willy Bett kwenye baraza jipya la mawaziri, huku akitarajiwa kutoa orodha kamili ya watakaopeperusha bendera katika awamu yake ya pili na ya mwisho uongozini.

latest stories