Omamo na Matiang’i wakanusha KDF watatumiwa
Published on: July 29, 2017 08:27 (EAT)
Audio By Vocalize
Mawaziri Raychelle Omamo wa ulinzi na mwenzake Fred Matiang’i wa usalama wa ndani wamekanusha madai ya muungano wa Nasa kuwa serikali inapanga kuwatumia wanajeshi kuiba kura katika uchaguzi mkuu ujao. Wakihutubia waandishi wa habari mjini Kisumu mawaziri hao walisema kuwa nia ya muungano wa Nasa ni kuzua hofu miongoni mwa wakenya kwani madai yao hayana msingi wowote.


Leave a Comment